Header Ads Widget

RC SIMIYU AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA KUPOZEA UMEME WA GRIDI YA TAIFA.

 



Na COSTANTINE MATHIAS-Simiyu.


MKUU wa  Mkoa wa Simiyu Anamringi Macha, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha kupoozea umeme wa gridi ya Taifa unaojengwa katika Wilaya za Maswa, Itilima na Bariadi Mkoani humo.


Mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi Bil. 90, unajengwa Mkoani humo ili kuondoa changamoto ya uhaba na kukatika katika Kwa Umeme jambo ambalo lilikuwa linakwamisha Shughuli za Maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda.


Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa mradi huo, Mkuu huyo wa Mkoa amemuelekeza Mkandarasi KARPATARU PROJECT INTERNATIONAL LTD anayetekeleza mradi huo kuhakikisha kuwa anakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa ili Wananchi waweze kunufaika na umeme wa uhakika wa Gridi ya Taifa.


Aidha Macha ameuelekeza Uongozi wa Shirika la Ugavi wa umeme Nchini (TANESCO), kuhakikisha kuwa wanamsimamia kwa karibu mkandarasi huyo ili aweze kukamilisha mrsdi huo kwa wakati


Mwisho.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI