Na Odero Odero
Serikali ya Kongo inazungumza na waasi wa M23,Serikali ya Kongo inazungumza na Serikali ya Rwanda.
Serikali ya Urusi inazungumza Serikali ya Ukraine Israel na Palestina wanazungumza Historia yetu pia inaonesha kwamba CCM na CUF waliwahi kuzungumza na kuridhiana.
Serikali ya Tanzania chini ya Jakaya iliwahi kuzungumza na CHADEMA na mazungumzo yalizaa mchakato wa Katiba Mpya japo hatukufika mwisho.
Rais Samia aliwahi kukutana na kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bwana Tundu Lissu akiwa Ubelgiji- Mazungumzo yao yalifungua fursa ya Lissu kulipwa mafao yake ya kibunge na kuhakikisha usalama wake akirejea nyumbani baada ya kukimbia nchini mwakan2020 ,Mwenyekiti Mbowe kuachiwa huru.
Rais Samia aliwahi kukutana na Mwenyekiti wa CHADEMA Bwana Freeman Mbowe - Mazungumzo yao yalizaa matunda ya kuanzishwa kwa mazungumzo ya maridhiano baina ya Serikali,CHADEMA na CCM (Wafungwa zaidi ya 400 walifutiwa mashitaka na kuwa huru,waliokimbia nchini akiwemo Lissu,Wenje,Lema walirejea nyumbani, walau mazingira ya ufanyaji wa siasa yalianza kuwa rafiki)
Maalim Seif Sharif Hamad ( Marehemu) aliwahi kuzungumza na Amani Karume (Rais wa Zanzibar kwa wakati huo) mazungumzo yao yalizaa marekebisho makubwa ya Katiba ya Zanzibar na kuasisiwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)
CHADEMA, NCCR- Mageuzi,NLD, CUF mwaka 2015 walizungumza ,wakazika tofauti zao na kusimamisha mgombea moja wa Urais na matokeo yake tuliona.
Dr Slaa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye wakati moja alitofautina na CHADEMA na kuamua kukaa pembeni mwaka huu 2025 amezungumza na CHADEMA na ameamua kurejea na sasa ni mwanachama na kada mtiifu wa chama ambaye kwenye oparesheni za kudai Mageuzi ya Mfumo wa Uchaguzi alikuwa mstari wa mbele.
Mzee Wassira ,wakati moja alikimbia chama chake cha CCM na kujiunga na Upinzani alifanya maridhiano na chama chake na leo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara
Dr Emmanuel Nchimbi wakati moja hakukubalina na chama chake kuhusu mchakato wa uteuzi wa mgombea Urais akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu pamoja na wenzake walitoka hadharani na kutofautiana na Mwenyekiti wa chama wakati huo Bwana Kikwete ,lakini Nchimbi leo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya mazungumzo na kuridhiana ndani ya chama.
Baada ya kuonesha walau mifano michache kuhusu Maridhiano, Mapatano na kuanza upya ,ninauliza:
Ni nini kinazuia Vyama vya siasa kukutana na kuzungumza, kuridhiana na kufungua ukurasa mpya baada ya yaliyotokea Oktoba 29 ?
Kwa nini Rais Samia asikutane viongozi wakuu wa vyama vya siasa nchini na kufanya mazungumzo ili kufungua njia kwenda kwenye maridhiano ya Kitaifa?
Kwa nini Viongozi wa Dini mbalimbali nchini wasikutane na Rais kufanya mazungumzo ili kufungua njia ya mazungumzo ya maridhiano nchini?
Kwa nini Rais Samia asifanye mikutano walau miwili au mitatu na Vijana kwa njia ya Mtandao ili kuzungumza na Vijana na kuanza kufungua mlango wa mazungumzo ya maridhiano? Napendekeza jina la program liitwe One to One na Madam President.Program iwe live kwenye Tvs ,Social Media
Kwa nini Viongozi wa Wilaya na Mikoa wasianze kufanya mikutano ya kuwasikiliza Vijana kwenye maeneo yao ili kufungua mlango wa mazungumzo ya maridhiano?
Kwa nini Ma OCS OCDs,RPC,IG wasianze kukutana na viongozi wa siasa kwenye maeneo yao ili kuzungumza nao na kufungua mlango wa mazungumzo ya maridhiano badala ya kuamua kutizama kama paka na panya ?
Mazungumzo, Mazungumzano ni TIBA ya mkwamo wetu.
Unyenyekevu ,Unyenyekevu, Unyenyekevu ni Mlango wa Maridhiano.
#Mbele Kuna Mwanga
imetolewa na Odero Odero Balozi wa Aman

.jpg)





0 Comments