Header Ads Widget

MWIGULU AAGIZA MADEREVA WA SERIKALI KUHESHIMU SHERIA ZA BARABARANI

 


Na Matukio Daima Media ,Dodoma

Waziri Mkuu Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameonesha kukasirishwa na namna ambavyo Magari ya serikali yanaongoza katika kuvunja sheria za usalama barabarani, akiagiza Maafisa wa serikali kufuata sheria hizo ama kutoa mapendekezo ya sheria hizo kubadilishwa.


Mhe. Nchemba amebainisha hayo leo Jumatano Novemba 26, 2025 wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya kwanza ya wiki ya usafiri endelevu ardhini, Hafla iliyofanyika Jijini Dar Es Salaam, akibainisha tabia ya mwendokasi na kutoheshimu sheria na alama za barabarani kwa madereva wa magari ya serikali.

"Mhe. Waziri wa uchukuzi kaeni wadau wote mnaohusika ikiwemo Polisi, kama tunaona Vibao, spidi na sheria nyingine za usalama barabarani zimepitwa na wakati tuzibadilishe kama hazitekelezeki ili tuweke zile tunazotumia." Amesema Dkt. Mwigulu.

Waziri Mkuu ametaka kusiwe na sheria za wananchi wa kawaida na kuwa na sheria ama taratibu za serikali barabarani, akihoji ikiwa sheria na taratibu za barabarani zinakera madereva na watumiaji wengine wa barabara ni nani atakayepaza sauti kueleza changamoto hizo za sheria za usalama barabarani.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI