Header Ads Widget

MAENDELEO NA USTAWI WETU UNATEGEMEA AMANI NA UTULIVU- PM NCHEMBA

 


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesisitiza umuhimu wa kuendeleza kuimarisha amani nchini na utulivu, akisema maisha na uhai wa Kila Mtanzania unategemea uwepo wa amani na utulivu katika ustawi na maendeleo binafsi na ya Taifa.


Mhe. Mwigulu amebainisha hayo leo Jumatano Novemba  26, 2025 wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Kwanza ya Wiki ya usafiri endelevu ardhini, Mkutano uliofanyika Jijini Dar Es Salaam ukiongozwa na kaulimbiu isemayo "Nishati safi na ubunifu katika usafirishaji."


"Niwaombe Watanzania, niwaombe Vijana wenzangu tuimarishe amani na utaratibu wetu wa kushughulikia mambo yanayohusu Taifa letu." Amesisitiza Mhe. Waziri Mkuu.


Katika maelezo yake, Waziri Mkuu ameeleza kufurahishwa na baadhi ya hotuba za washiriki wa mkutano huo kutoka nje ya nchi, ikiwemo namna ambavyo Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye ujenzi wa miundombinu, ikiwemo rekodi ya kuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kwa kuwa na reli ndefu zaidi ya kisasa na Miongoni mwa nchi tano zenye reli ya kisasa duniani, akisema mafanikio hayo yasingeweza kufanikiwa bila ya uwepo wa amani nchini.


Amesisitiza kuwa haiwezekani kufikia mafanikio yaliyofikiwa kwenye miundombinu na sekta nyingine muhimu bila ya uwepo wa amani, akisema matukio ya uvunjifu wa amani ni sehemu ya jitihada za kutaka kuirudisha nyuma Tanzania katika maendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI