Header Ads Widget

MISA -TAN YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI JUU YA UANDISHI WA HABARI ZA AMANI.

 

NAIBU Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani, Denis Londo amefungua Mafunzo ya siku moja kwa Waandishi wa Habari za Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA), kuhusu Uandishi wa Habari za Amani (Peace Journalism Training) ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Morena Hotel Jijini Dodoma.


Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.


NAIBU Waziri, Wizara ya  Mambo ya Ndani, Denis Londo amefungua Mafunzo ya siku moja kwa Waandishi wa Habari za Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA), kuhusu Uandishi wa Habari za Amani (Peace Journalism Training) ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Morena Hotel Jijini Dodoma.


Mafunzo hayo ambayo yamewakutanisha waandishi wa habari 100 kutoka mikoa mbalimbali nchini, yameandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika – Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), yakilenga kuwajengea uwezo waandishi katika Uandishi wa Habari wa Amani — aina ya uandishi unaolenga kuimarisha utulivu, kuzuia uchochezi, na kuripoti kwa namna inayojenga maelewano na mshikamano katika jamii.


Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Londo amesisitiza kuwa waandishi wa habari wana nafasi muhimu katika kulinda umoja wa kitaifa kupitia matumizi ya lugha inayojenga, utoaji wa taarifa sahihi, na kuepuka taarifa zinazoweza kuchochea migogoro, hususan katika nyakati nyeti kama chaguzi na migogoro ya kijamii.




Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema taasisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo ya aina hii ili kuhakikisha tasnia ya habari inaendelea kuchangia kikamilifu katika kudumisha amani na ustawi wa taifa, hususan baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Amesema mafunzo hayo yataongeza weledi na uelewa kwa Waandishi wa Habari, kupunguza taarifa zenye uchochezi, kuwajengea uwezo waandishi wa Habari kuchambua migogoro na kuleta suluhishi pia kuimarisha Umoja na mshikamano wa Taifa la Tanzania. 

Amebainisha kuwa licha ya kuwepo kwa lawama kutoka kwa baadhi ya watu wanaodai kuwa vyombo vya habari havijatekeleza wajibu wao ipasavyo, mtazamo huo hautoi picha sahihi ya kazi zinazofanywa na wanahabari kwa kujituma na kwa kuzingatia maadili.


Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Soko ameongeza kuwa MISA Tanzania itaendelea kutoa mafunzo ya aina hii ili kuhakikisha tasnia ya habari inaendelea kuchangia kikamilifu katika kudumisha amani na ustawi wa taifa, hususan baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.


Akiwasilisha Maada kuhusu, Constructive Journalism for Peace Highlight, Solution and Nonviolent Approaches, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Sauti, Dk. Dotto Bulendu amesema Uandishi wa HABARI imebadilika kulingana na Mazingira tofauti na zamani ambapo vyombo vya habari vililenga kusukuma Agenda za Maendeleo.


Mwisho.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI