Mwandishi wetu Matukio Daima Media Dodoma
Mbunge Mteule wa Monduli, Izack Joseph Copriano (Kadogoo), ashiriki kikao cha kwanza cha Bunge la 13 jijini Dodoma huku akiwa na Ari mpya kuwatumikia wakazi wa Monduli.
Izack Joseph Copriano, maarufu kama Kadogoo, Mbunge mteule wa Jimbo la Monduli (CCM), leo tarehe 11 Novemba 2025, ameshiriki kwa mara ya kwanza kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachoendelea jijini Dodoma.
Kikao hiki ni sehemu ya Bunge la 13, ambacho kimeanza leo na kujumuisha wabunge wapya pamoja na wale waliorejea, wakitarajiwa kuapa katika siku chache zijazo kabla ya kuanza rasmi majukumu yao.
Kadogoo, ambaye kabla ya kugombea ubunge aoikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli alipata ushindi wake wa kishindo Oktoba 29, 2025, ameonekana akiwa na ari, nidhamu na hamasa kubwa ya kulitumikia Taifa, huku akisisitiza dhamira yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Monduli .
Katika kampeni zake miongoni mwa ahadi zake zikizompa ushindi ni kutatua kero ya maji na kumaliza migogoro ya ardhi Monduli huku akiahidi kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za afya lakini pia suala la elimu likiwa kipaumbele kikubwa.








0 Comments