Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Jackson Kiswaga leo Machi 12, 2026 imewasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa ajili ya ziara ya kutembelea Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) katika Halmashauri ya Iringa.
Wajumbe hao wameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Balozi Baraka Luvanda na watendaji kutoka Ofisi hiyo.
Akizungumza, Dkt. Dugange alisema mradi huo unawezesha wananchi kufanya shughuli za kiuchumi bila kuathiri mazingira.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James alipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa utekelezaji wa mradi huo na kusema unasaidia kulinda mazingira.
Mradi huo pia unatekelezwa katika Halmashauri za Wilaya za Wanging’ombe, Mbarali na Mbeya katika bonde la Ruaha Mkuu na halmashauri za Sumbawanga, Mpimbwe na Tanganyika katika Bonde la Ziwa Rukwa











0 Comments