
Hata hivyo, Lukuvi amesema alitambua angekalia kiti cha Spika kabla ya kuchaguliwa kwa Spika mpya ambaye atakwenda kukalia kiti hicho.
.
Lukuvi amepewa heshima hiyo ambapo kanuni huwa zinamruhusu Mbunge aliyekaa bungeni kwa muda mrefu mfululizo.
Mbunge huyo aliingia kwa mara ya kwanza bungeni mwaka 1995 ambapo kulikuwa na uchaguzi wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi.
"Naomba kufuta uvumi ambao ulienea mitandaoni kuwa nimegombea kiti cha Spika, naomba niseme sikugombea na sikutamani kugombea, ila nilijua ningekalia kiti hiki kama 'Spika' wa kwanza kabla ya Spika atakayechaguliwa," amesema Lukuvi.
Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wapiga kura wa jimbo lake kwa jinsi walivyomchagua kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.






0 Comments