Na Matukio Daima Media
Maendeleo JOPO la mawakili wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na (CHADEMA) Tanzania Bara, John Heche, limeomba Mahakama Kuu kutoa muda wa siku tatu ili kufanya utafiti na kujipanga ku jibu mapingamizi yaliyowasilish-wa na upande wa Jamhuri katika kesi ya kushikiliwa kwa kiongozi huyo.
Ombi hilo liliwasilishwa jana mbele ya Jaji Obadia Bwegoge na jopo la mawakili wa Heche lin-aloongozwa na Selamani Matau ka, likijumuisha Fredrick Msacky, Paul Kisabo, Neema Salum, Dorice Kafuku na Maduhu Wil-liam.
Mawakili hao waliwasilisha maombi ya mahakama kuamuru Heche ama afikishwe mahakamani au aachiliwe kwa dhamana, wakieleza kuwa kushikiliwa kwake bila kufikishwa mahakam ani ni kinyume cha sheria.
Wajibu wa maombi hayo ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanza-nia, Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni (RCO), Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Mwa nasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Awali, Wakili wa Serikali Mkuu Agatha Pima aliieleza mahakama kuwa upande wa Jamhuri ume-peleka pingamizi la awali dhidi ya maombi hayo na tayari taarifa ya pingamizi imeshawasilishwa kwa upande wa waleta maombi.
"Upande wa wajibu maombi tulipewa nafasi ya kujibu kiapo kinzani. Kwa kuwa juzi ilikuwa Jumapili, tumewasilisha taarifa ya kiapo leo (jana). Hata hivyo,
kabla hatujaendelea na majibu, tumeleta pingamizi la awali." al-idai Wakili Pima.
Baada ya maelezo hayo, Wakili Matauka alidai kuwa taarifa ya pingamizi la awali wameipokea nusu saa kabla ya kuanza kwa kikao, hivyo kuhitaji muda wa kufanya utafiti wa kisheria na kuandaa majibu.
"Ni maombi yetu kwa heshima kwamba kutokana na pingamizi hilo jipya, tupatiwe muda wa siku tatu kujiandaa hadi Novemba 13, 2025," alisema Matauka.
Baada ya kusikiliza pande zote. Jaji Bwegoge alikubaliana na ombi hilo na kuelekeza kuwa shauri hilo litaendelea Novemba 13, 2025 saa 4:30 asubuhi.
"Kwa kuwa waleta maombi wenyewe wameomba muda wa kujiandaa. Mahakama inaridhia ombi hilo," alisema Jaji Bwegoge. Heche alikamatwa na kushi-
kiliwa na jeshi la Polisi tangu Oktoba 22, 2025, alipokuwa nje ya geti la Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyo-tolewa na Wakili Hekima Mwa-sipu tarehe Novemba 4, 2025, Heche anatuhumiwa kujihusi-sha na vitendo vya kigaidi katika maeneo ya Kimara, Magomeni, Msewe na External.
Hata hivyo, juzi jioni, Jeshi la Polisi liliwaachia kwa dhamana Heche na viongozi wenzake wa CHADEMA waliokuwa wanashi-kiliwa.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kamata mtuhumiwa, anapaswa (CPA), askari polisi anapom-ama amfikishe mahakamani nda-ni ya saa 24 au kumwachia huru, isipokuwa kwa tuhuma ambazo zinahusiana na makosa yenye adhabu ya kifo.






0 Comments