Header Ads Widget

JESHI LA POLISI LAWASAKA WANAOHAMASISHA KUVURUGA AMANI YA NCHI


 Jeshi la Polisi Nchini limetoa tahadhari kali kwa makundi na watu binafsi wanaotoa kauli, matangazo au mikutano inayoweza kuhatarisha amani na kuibua chuki miongoni mwa Wananchi, likisisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.


Katika taarifa iliyotolewa leo tarehe 21 Novemba 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi jijini Dodoma, jeshi hilo limesema linaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa hali ya usalama nchini, hususan katika kipindi hiki ambacho kumeshuhudiwa ongezeko la matamko yanayodaiwa kuashiria kuvuruga utulivu wa nchi.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya watu na makundi yamekuwa yakijitokeza kutoa misimamo na kauli zinazolenga kueneza chuki, hivyo Jeshi hilo linaendelea kuchukua hatua


kwa mujibu wa SheriaTaarifa hiyo imesomeka "Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua kwa matamko na matendo yote yenye lengo la kuchochea chuki na vurugu nchini wakati huu ambao nchi ikiwa na jukumu kubwa la kuleta maridhiano ili kulinda amani na utulivu na kuendelea kukuza uchumi wetu kwani kukitokea vurugu kila mmoja wetu atapata athari hasa kiuchumi, kijamii na kiusalama"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI