Amir Japhari, Fundi Magari anayefanya shughuli zake za ufundi Mkoani Dar Es Salaam, amesisitiza kuwa machafuko na matukio ya uvunjifu wa amani nchini hayawezi kuwa mbinu ya upatikanaji wa haki kwa baadhi ya watu, akihimiza kila Mtanzania kuilinda amani badala ya kukimbilia kufanya fujo zisizokuwa na faida yoyote.
Japhari akizungumza na Chombo chetu cha habari mapema leo Jumanne Novemba 25, 2025, amemshukuru Rais Samia pia kwa kusikia kilio cha Vijana na kuunda wizara ya maendeleo ya Vijana pamoja na kuteua Mawaziri wengi Vijana, akiamini kuwa Viongozi hao wanafahamu na wana uwezo mkubwa wa kushughulikia changamoto za Vijana nchini.
"Amani ni kitu muhimu sana katika Taifa hili, Vijana wengi wanafikiri Taifa hakuna linachowafanyia lakini ukiangalia kuna Mataifa mengi yameingia kwenye machafuko wakiamini kuwa ndio chanzo cha kupata haki zao leo wamefika sehemu wanatamani amani na imekuwa ngumu kuirejesha.
... Leo ukiangalia katika nchi yetu, tulipotoka na tunakoelekea mimi naona tunakoelekea ni kuzuri zaidi kwasababu huko nyuma changamoto za kimaisha zilikuwa nyingi zaidi lakini kwasasa tumejitahidi sana kwenye maendeleo tofauti na Vijana wanavyoona." Amesema Bw. Japhari.





0 Comments