Mwenyekiti wa Taasisi ya Al- Hikma Islamic Foundation Sheikh Nurdin Kishki amesema wajibu wa viongozi wa dini kote nchini ni kusimamia Amani na mshikamano wa jamii pamoja na kuonya wananchi wasikubali kutumika kwa maslahi binafsi ya watu wanaotaka kuvuruga mshikamano na amani ya Tanzania.
Sheikh Kishki ameyasema haya Leo Jumatatu Oktoba 27, 2025 kwenye kongamano la viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali lililofanyika jijini Dar es Salaam, Ajenda kuu ikiwa ni kuilinda na kuitunza amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano ya Oktoba 29, 2025.
Kishki amezungumzia pia tabia iliyozuka nchini kwa baadhi ya watu wanaowakebehi na kuwasema Viongozi wanaosema mema ya nchi na kuelekeza kuhusu amani na mshikamano wa Watanzania kwa madai kuwa wanafanya hivyo kutokana na kuwa wanalipwa fedha na Mamlaka.





0 Comments