Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine kusherekea siku ya Mbolea Duniani kila Oktoba 13 Ya Mwaka,Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini TFRA imesema Matumizi ya Mbolea tangu kuanzishwa kwa Ruzuku yameongezeka Toka Zaidi ya Tani laki Tatu Hadi Tani laki Tisa.
Katika Kijiji Cha Ujindile kata ya Igosi wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe kulikofanyika sherehe za siku ya Mbolea Kitaifa mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Bwana Joel Laurent anasema ongezeko Hilo limesaidia kuongeza tija kwenye chakula Hadi nchi kuwa na Ziada ya chakula.
Baadhi ya wakulima wa viazi,Mahindi na Parachichi wilayani Wanging'ombe akiwemo Elly Chengula,Shadrack Mligo na Israel Mwalongo wanasema licha ya kukiri kusaidika na Mbolea za Ruzuku lakini uhaba wa maji umekuwa mwiba mkali kwao huku wakiomba kuchimbiwa visima katika Mashamba yao.
Kwa Upande wake Ofisa Kilimo mkoa wa Njombe Wilson Joel anasema Matumizi ya Mbolea kwa wakulima imesaidia kuwa na Ziada ya chakula katika mkoa.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na Kampeni ya kuwaelimisha wakulima juu ya Matumizi sahihi ya Mbolea kwa Kauli mbiu ya Mali shambani,Silaha Mbolea.
0 Comments