Header Ads Widget

DIWANI WA IYELA AHAIDI KUWATUMIKIA WANANCHI KWA KASI NA UADILIFU.

 


Na SAMWEL MPOGOLE - Mbeya.


DIWANI wa Kata ya Iyela, Mheshimiwa Abisalom Mwambepo, ameahidi kuwatumikia kikamilifu wananchi wa kata hiyo kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu na kuhakikisha ahadi alizotoa wakati wa kampeni zinatimia kwa vitendo.


Akizungumza mara baada ya kuapishwa rasmi, Mheshimiwa Mwambepo alisema kuwa wananchi wa Iyela wamempa dhamana kubwa ambayo ataithamini kwa kufanya kazi kwa bidii, uwazi na ushirikiano wa karibu na wananchi pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali.



Amesisitiza kuwa vipaumbele vyake vitajikita katika kuboresha miundombinu, kuinua sekta ya elimu, afya, pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao ya kila siku.


Kwa upande wao, wananchi wa Kata ya Iyela hawakuficha furaha yao baada ya kumpata kiongozi huyo mpya na wameeleza kuwa wana imani kuwa chini ya uongozi wake, kata hiyo itapiga hatua kubwa katika maendeleo na ustawi wa jamii.


Ezekiel Kibonde amesema wanaamini diwani wao mpya ataendeleza juhudi za kupambana na changamoto za barabara na huduma za kijamii, akiwapongeza wananchi kwa umoja waliouonyesha.


 Sophia Samsoni ameeleza kuwa uteuzi huo umewapa matumaini mapya, hasa katika suala la kuinua wanawake na vijana kiuchumi.


Naye Ernest Kayombo ameahidi kushirikiana kwa karibu na diwani huyo katika masuala ya maendeleo, akibainisha kwamba mafanikio ya kata hiyo yatategemea ushirikiano wa wananchi.


Mwisho.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI