Header Ads Widget

MHE LT.JEN.MSTAAFU BALOZI YACOUB MOHAMED AMEIKARIBISHA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA OFISI ZA KONSELI JIJINI DUBAI


Mheshimiwa Lt. Jen. Mstaafu Balozi Yacoub Hassan Mohamed, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ameikaribisha rasmi timu ya Taifa ya Tanzania katika Ofisi za Konseli Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dubai.

Timu ya taifa ya Tanzania iliwasili Dubai alfajiri ya Tarehe 12 Oktoba , 2025 ikitokea kwa aiji ya pambano la kirafiki na Timu ya Taifa ya Iran utakafanyika tarehe 14 Oktoba,2025.

Mheshimiwa Balozi Yacoub pamoja na mambo mengine  aliwasisitiza viongozi na wachezaji wa timu hiyo kuzingatia nidhamu ya mchezo na wapambane  uwanjani ili watoke na ushindi.
.
Sambamba na hilo Mheshimiwa Balozi Yacoub, aliipongeza timu ya Taifa kwa kuendelea kuimarika kadri ya siku zinavyoenda na kuutaka uongozi kutumia fursa za kujipima uwezo kwa kushinda kila mechi ili ipande chati katika orodha rasmi ya FIFA.

Kwa upande wake Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Hemed Seiman Morocco alimshukuru Mheshimiwa Balozi kwa maandalizi mazuri ya uratibu kuanzia siku ya mapokezi hadi wakati huu na kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono sekta ya michezo hususan mpira wa miguu na timu ya taifa kwa ujumla.

Kocha Morocco alitoa shukrani za kipekee kwa namna maandalizi ya mapokezi yao na mwaliko  katika ofisi za Konseli kuu ulivyoratibiwa na kueleza kuwa wameshasafiri nchi nyingi lakini mapokezi ya Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu ni ya kipekee na ya hali ya juu kabisa na haikuwahi kutokea kupata  ukarimu wa aina hiyo nchi zote walizosafiri awali.


Kocha Morocco ameomba ushirikiano wa namna hiyo uendelee kufanyika katika maeneo yote Timu ya Taifa itaposafiri na kueleza kuwa jambo hilo limeifanya timu hiyo kujisikia ipo katika mikono salama na kupata motisha zaidi ya kupambana na kuhakikisha ushindi unapatikana.

Amesema Timu ya Taifa ya Tanzania ipo katika hali nzuri kiafya na kimchezo na kumtaka na kwamba Watanzania wategemee burudani safi siku ya mchezo huo.

Aidha Uongozi wa Timu ya Taifa kupitia Kocha mkuu wa Timu hiyo Ulimkabidhi Mheshimiwa Balozi Jezi ya Timu ya Taifa ya Tanzania ikiwa ni kama kumbukumbu yake



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI