Header Ads Widget

WAGOMBEA UBUNGE, UDIWANI (CUF) WAAHIDI KUTATUA KERO YA MAJI NA BARABARA.

 


Na Josea Sinkala, Mbeya.

Mgombea udiwani wa kata ya Itezi jimbo la Uyole kupitia Chama cha Wananchi CUF Erasto Swalo, ameeleza kusikitishwa na hali ya kata ya Itezi na maeneo mengine ya Uyole kukosa huduma ya uhakika ya maji safi.

Swalo amesema ni masikitiko kuona kata yake haina huduma ya kutosha ya maji safi hivyo kuwashukuru waliochimba visima na kuwauzia maji wananchi katika kupunguza adha ya upatikanaji huduma hiyo kwa wananchi.


Mgombea huyo wa udiwani amewaomba wananchi kumchagua awe Diwani wa kata ya Itezi ili kwenda kuhoji Serikalini juu ya tatizo hilo la muda mrefu pamoja na kero nyinginezo ikiwemo ubovu wa barabara za Itezi.

Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Uyole kupitia Chama hicho bwana Ibrahim Mwakwama, amewaomba wananchi kumchagua awe mbunge wao ili kuhakikisha anawaunganisha wananchi wa Uyole kuzungumza lugha moja na kukemea matukio ya utekaji na mauaji ya watu yanayosikika katika maeneo mbalimbali nchini.


Mwakwama amesema pamoja na kuwaunganisha wananchi wake lakini atahakikisha upatikanaji wa huduma ya maji unaimarishwa, kujengwa kwa kituo kikubwa cha mabasi jimbo la Uyole na kuhakikisha fedha ya mfuko wa jimbo inatatua kadhia zote kwenye sekta ya elimu.

Haya yanajiri kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 ambapo vyama mbalimbali vya siasa vinaendelea kunadi sera zake kwa wananchi huku chama kikuu cha upinzani CHADEMA kikiwa hakishiriki uchaguzi huo kutokana na mashinikizo yake makubwa ya kutaka mabadiliko ya sheria za kiuchaguzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI