Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
VIONGOZI wa madhehebu ya dini Mkoani Simiyu wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani kupitia nyumba za ibaada ili waumini wao waweze kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani.
Akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya amani kilichofanyika katika ukumbi wa Bariadi Conference, aliyekuwa Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu amewataka viongozi wa dini kutumia sauti na Imani zao kuhubiri amani.
Alisema kuwa Viongozi wa dini wana nguvu kubwa ambayo Mungu amejalia, ambapo wakiitumia vyema Tanzania itavuka kwenye Uchaguzi kwa amani sababu imani zimejenga toka mbali na zina historia kubwa.
"Tunaingia katika Uchaguzi ambayo ni wa kwanza katika kizazi ambacho kimeshamiri kwenye matumizi ya kidigitali...Wengine wanatumia vibaya mitandao ya kijamii na wengine wanatumia vizuri, Nchi yetu imepita mitihani ya udini na ukabila, Sasa tunakwenda kuvuka mitihani ya Uchaguzi" amesema Nyarandu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, AnaMringi Macha, amesema kuwa amesema kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekamilisha kufanya maandalizi yote ya Uchaguzi, huku akiwahakikisha Uchaguzi itafanyika kwa amani na usalama.
"Tumeitana hapa leo na tunachoomba kwenu ni kuliombea Taifa na ushuhuda wenu, mna nguvu kubwa ya kuaaminisha watu mnaowahubiri...Niwahakikishie katika Mkoa wetu, uko salama, kwa kadri ya uwezo wetu na nguvu za Mungu, tutafanya Uchaguzi kwa amani na usalama_ amesema.
Mkuu huyu wa Mkoa aliwaonya watu wenye nia ovu kuacha kutumika vibaya ambapo amesisitiza "Kuna Watu wachache wenye nia mbaya ya kutumia mitandao vibaya, wenye nia ovu, sumu haijalibiwi kwa kuonja, twende tukapige kura wala tusiweke viongozi wa kujaribu."
Mwenyekiti wa Kamati ya amani Mkoani humo, Shekhe Isa Kwezi amesema kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kusema na kuwaambia watu kuwa hatuna nchi nyingine ya kwenda zaidi ya Tanzania endapo yakitokea machafuko.
Alisema viongozi wa dini watakuwa na dhambi kubwa sana endapo hawatahubiri amani na kusisitiza Elimu itolewe ili watu wasiwe na hofu ya mtazamo siku ya kupiga kura na vyombo vya ulinzi na usalama wawepo kwa ajili ya kulinda usalama na kuwalinda wananchi.
"Nchi hii haitochafuka sababu ya ukabila, maana tuna makabila mengi, siku ikichafuka viongozi wa dini au wanasiasa Watakuwa wamehusika...Tufanye ibada huku tukiwa na amani, 29.10.2025 ni siku ya uchaguzi, tuhimize watu wakapige kura" amesema Shekhe Kwezi.
Yasin Lema, mwakilishi wa kundi la Vijana amesema kuwa kundi hilo linatumika sana kutengeneza mambo ambayo hayafai na kuwasisitiza vijana wasitumike vibaya kubaribu amani iliyopo.
Aliwataka vijana kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kulinda amani ya Tanzania pia akiwasisitiza washiriki kupiga kura pia waheshimu maanuzi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi juu ya Matokeo yatakayotanganzwa.
Mwisho.









0 Comments