Header Ads Widget

USALAMA UMEIMARISHWA NCHI NZIMA, TUJITOKEZE KUPIGA KURA BILA HOFU — BASHUNGWA

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, amewahakikishia Watanzania wote kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa nchi nzima, hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki kupiga kura kuwachagua Rais, Wabunge na Madiwani bila hofu yoyote kesho, tarehe 29 Oktoba 2025.

Bashungwa ameyasema hayo leo, tarehe 28 Oktoba 2025, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaifa, ikiwa ni siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

“Kesho, Oktoba 29, hakutakuwa na shida yoyote. Vyombo vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi, vipo timamu nchi nzima. Usalama umeimarishwa, kwa hiyo Watanzania tuende tukapige kura bila kuwa na wasiwasi wowote. Na yeyote atakayethubutu kuvuruga amani, atakutana na kisiki,” amesisitiza Bashungwa.

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa vijana kujitokeza kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo, akiwataka pia kujiepusha na vitendo au vishawishi vyovyote vinavyoweza kuvuruga amani, akisisitiza kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imebainisha fursa nyingi mahsusi kwa ajili ya vijana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI