Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio DaimaMedia
UMOJA wa makanisa ya kitume na kinabii Tanzania imefanya ibada maalumu ya maombi kwa Taifa katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29,2025 huku ukikemea baadhi ya viongozi wa dini wanaochochea vurugu na kuhamasisha maandamano kwa wananchi.
Akiongoza ibada hiyo maalumu ya maombi iliyofanyika katika kanisa la Sauti ya Uponyaji mkoani Morogoro ,Rais wa umoja wa makanisa hayo Nabii Joshua Aram Mwantyala alisema Kila Taifa duniani una utamaduni wake kwa maana ya Mila na desturi na utamaduni unajengwa na jinsi uumbaji wa kieneo ulivyo.
Nabii Joshua alisema kwa bara la Afrika haikanushiki kwamba Tanzania ndio baba na kiongozi wa wa Amani kwani Tanzania ilipata uhuru kwa njia ya mazungumzo kati ya waasisi wa Taifa na wakoloni waliokuwa watesi wa Taifa letu.
"Utamaduni huu umejengwa na tumeurithi na kwa kuwa ni utamaduni mzuri ni rai kwa watanzania tukauenzi na kuuendeleza na Dunia ijue kuwa Tanzania mambo yao uwa wanamaliza kwa mazungumzo na sisi asili yetu ni ndugu,"alisema.
Aidha alisema inapotokea baadhi ya watu wananajisi utamaduni huo nankutaka tupate maelewano kwa njia ya mafarakani wasikubaliwe kamwe na badala yake wakatae na kukemea.
"Zimebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 tufuate kanuni na Sheria za nchi, mtu yeyote anayesimama na kupinga uchaguzi wa kikatiba ananajisi utamaduni,katiba na Sheria za nchi huyo pia tusimkubalie kamwe, tudumishe Amani ya nchi yetu kwa kukataa kabisa njia za vurugu kwamba zinaweza kutengeneza mshikamano na sio utamaduni wetu na si asili yetu,"alisema.
Akazungumzia manabii wanaotabili vurugu na machafuki kwenye nchi ya Tanzania, alisema hana maana ya Kupambana nao lakini kwa dhamana aliyonayo kama nabii wenzao aliwaeleza kuwa Mungu ni wa amani na aridhii matangazo ya machafuko, manabii wote wanaotabili mambo yanayoamasisha watu kutoka nje na kufanya maandamano kupinga Sheria za nchi na katiba ya nchi hawatokani na Mungu.
Alisema manabii wote waliotokana na Mungu wamekuwa wakiheshimu Mamlaka na taratibu zilizowekwa kwenye jamii yao, hakuna haja ya kutafiti kinachoangaliwa kinachotabiliwa hakipo kwenye msingi hivyo kuna Kila sababu na kukemea.
"Wapo wanaolipwa fedha ili wakatabili mabaya kwenye bibilia yupo nabii alilipwa ili wakatabiri mabaya ,watanzania msikubali kamwe kuondoa Amani ya nchi kwa mikono yetu wenyewe hatutapata uwezo wa KUREJESHA amani, viongozi wetu wa kisiasa,kijamii na dini walisha tuwekea misingi,lakini tunawaomba viongozi wetu wa kiasiasa rudini kwenye meza ya mazungimzo na kwenye msingi na nchi yetu tutakuwa tunaitendea haki,tuna haki kuwa na amani na kuishi kwa umoja,wacheche wasiharibu haki ya wengine,"alisema.
Mtume Fotunata Andengenye katika ibada hiyo alisema ni raia mwema wa mbinguni ni raia mwema wa Tanzania ,akawasii watanzania kutopoteza Amani ambayo imetolewa na Mungu.
"Uchaguzi ni wa muhimu tuwekeze kwa tamaduni zetu,kama Taifa tunachokitaka ni utulivu, wanawake tuwe wa kwanza kama silaa kugombea Taifa na familia na kukemea kusiwepo na maandamano,naombea viongozi wetu Rais,Wabunge na madiwani,"alisema.
Askofu mkuu wa kanisa la Bethel Calvary askofu Dk Willy Ackyoo alitolea mfano wa neo la bibilia kutoa Warumi 10:3.mara nyingi watu wamekuwa hawajui haki yao wenyewe wala ya Mungu.
Dk Ackyoo alisema katika wigo wa kikristo lazima kuongeza kama Wana wa kristo,akawataka watanzania kuwa makini katika kuitetea haki,kitakankuwa makini katika kunena na kuzungumza na kutumia vinywa vyao kutamka Amani kwani Amani ndo neno pekee linaloruhusu utulivu kwa nchi.
"Kama kuna wanaochochea kuwepo kwa maandamano sisi tutunze amani kama wapo wanaohimiza kuingia barabarani sisi tupande milimani kugombea Amani na Tanzania itavuka Salama,"alisema.
Mwisho.
0 Comments