Na mwandishi wetu
VIONGOZI wa Jamii ya Kimasai nchini Tanzania maarufu kama (Malaigwanan) wametoa tamko lao rasmi kwa nchi nzima, la kuunga Mkono kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025, wakilaani uwepo wa hamasa ya kufanyika kwa maandamano siku hiyo wakiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua Viongozi wanaowataka.
Viongozi hao wametoa tamko hilo katika eneo la Donyomorwak Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro kwenye Mkutano wao wa kawaida wa Orkiama ambapo akisoma tamko hilo kwaniaba ya Viongozi hao, Jeremia Laizer, Katibu wa Malaigwanani Tanzania, ameeleza pia kwamba Jamii hiyo itamuunga Mkono Kiongozi mwenye kutanguliza mbele maslahi ya wananchi pamoja na kulinda amani na utulivu wa Tanzania.
"Tunawahimiza wananchi wote kudumisha amani, mshikamano na utulivu, kuanzia ngazi ya shina, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda hadi Taifa zima, tukiepuka maneno ya uchochezi, migawanyiko, na fitina," .
"Tuchague maendeleo, umoja, na mustakabali mwema wa vizazi vya sasa na vijavyo. Tuwe nguzo ya amani, nuru ya matumaini, na urithi wa thamani kwa Taifa letu. Tanzania kwanza, amani kwanza." Amesema Bwana Laizer.
0 Comments