Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas
Sarkozy, ameanza rasmi kutumikia kifungo
cha miaka mitano gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kula njama ya kufadhili kampeni zake za urais mwaka
2007 kinyume cha sheria.
Mahakama imethibitisha kuwa fedha zilizotumika
kufadhili kampeni hizo zilikuwa zikitoka
kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya, marehemu Muamar Gaddafi.
Sarkozy mwenye umri wa miaka 70, anatarajiwa kutumikia kifungo chake katika Gereza la La Sante lililopo jijini Paris.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa zamani ameendelea kukanusha madai hayo,
akisisitiza kuwa hajawahi kujihusisha na uhalifu wowote unaohusiana na uchaguzi
huo.
0 Comments