Header Ads Widget

TBS KANDA YA KATI WAKAMATA NA KUTEKETEZA TANI 1.53 ZA BIDHAA HAFIFU ZA CHAKULA

 Na Adery Masta.

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza jumla ya tani 1.53 za bidhaa hafifu zenye thamani ya shilingi milioni Nane laki moja na elfu 10 , ambapo kati ya hizo Kuna bidhaa ambazo hazijakidhi matakwa ya Viwango na nyingine zimeisha muda wake wa matumizi, Zoezi hilo la uteketezaji limefanyika Jana Oktoba , 11 , 2025 Chidachi Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Afisa Udhibiti Ubora wa TBS Kanda ya Kati, Bw. Daniel Marwa alisema bidhaa hizo zilipatikana kupitia ukaguzi uliofanyika kuanzia Julai Hadi Oktoba 2025 katika mikoa ya Dodoma , Singida na Iringa .

Amezitaja bidhaa zilizokamatwa kuwa ni bidhaa za chakula ambazo hazikidhi viwango, pamoja na bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi.

“Tunawataka wafanyabiashara wa jumla kuacha tabia ya kuwauzia wafanyabiashara wa rejareja bidhaa zilizopitwa na muda wa matumizi kwa lengo la kuondoa bidhaa hizo sokoni, kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha afya za wananchi,” amesema Bw. Marwa

Aidha, amewataka walaji kuwa makini kwa kuhakikisha bidhaa wanazonunua zinakidhi matakwa ya ubora kwa kuangalia tarehe ya mwisho wa matumizi pamoja na alama ya ubora.

“Suala la usalama wa chakula ni mtambuka, kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa, kusambazwa na kuuzwa sokoni zinakuwa salama. Walaji wanapaswa kujiridhisha kabla ya kutumia bidhaa yoyote,” amesisitiza.

Kwa mujibu wa TBS, operesheni za ukaguzi na uteketezaji wa bidhaa zisizokidhi viwango zitaendelea nchi nzima ili kulinda afya za wananchi na kudhibiti biashara haramu ya bidhaa hafifu sokoni.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI