Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Shaweji Mkumbura akimnadi mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Mhe Tarimba Abbas katika uwanja wa kona Bar, Kijitonyama 11.10.2025. |
Na. Mwandishi Wetu,
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Tarimba Abbas amewahakikishia Wananchi wa Kata ya Kijitonyama kuwa wapo kwenye eneo la uchumi mkubwa kwa Dar es salaam ambapo kazi hiyo imewezeshwa na Serikali sikivu chini ya Chama hicho cha CCM.
Tarimba amesema hayo wakati wa muendelezo wa mikutano yake ya kampeni ya Kata kwa Kata, uliofanyika uwanja wa Kona Bar Kijitonyama, ambapo amenadi sera za Jimbo hilo pamoja na kumuombea kura za kishindo za Ndiyo, Rais Samia Suluhu Hassan na Diwani wa Kata hiyo Ndugu Amani Mohammed Barande.
Akinadi sera hizo, Tarimba amebainisha kuwa moja ya changamoto kubwa ambayo anaenda kuimaliza Bungeni watakapomchagua ni kwenda kulasimisha maeneo yote ya Jimbo la Kinondoni ili kuondokana na makazi yasiyo pimwa (Aquater).
"Mkitupa tiki Mimi Tarimba, Diwani Amani na Rais Samia Suluhu Hassan, hakuna kufeli kwani tutaendelea kuleta maendeleo.
Hizi barabara mnazoziona ikiwemo hii ya njia nne imejengwa wakati mimi nikiwa Diwani na tulilipitisha kwenye Halmashauri yetu ya Kinondoni, na sasa mnaona shughuli kubwa za kiuchumi Kata hii ya Kijitonyama.
"Kwa hapa Dar es salaam hakuna Wilaya yenye shughuli za kiuchumi kama Kijitonyama. Ajira zinapatikana kwa wingi na watu wanaoingia na kutoka ni wengi zaidi." Amesema Tarimba.
Aidha, amewahakikishia kuwa, Katika siku 100 za kwanza atakapokuwa Mbunge, atahakikisha anakaa na Diwani pamoja na makundi yote wakwele Vijana, Wa mama na wale wenye ulemavu ilikuwapatia nyezo za shughuli za kiuchumi.
Katika hatua nyingine, Tarimba amewaomba Wananchi wa Kinondoni kujitokeza kwa wingi siku ya Oktoba 21 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan atafanya mkutano viwanja vya Leaders club.
"Pia tarehe 21 Mama anakuja viwanja vya Leaders club, anataka kuzungumza na wana Kinondoni. Naomba mjitokeze kwa wingi sana. Ili tupate salamu za Mama" amemalizia Tarimba.
Kwa upande wake, Mgombea Udiwani wa Kata hiyo ya Kijitonyama, Ndugu Amani Mohammed Barande amewaomba wana Kijitonyama kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupiga kura kukichagua Chama Cha Mapinduzi CCM ilikuendelea kuleta maendeleo.
"Tunafahamu changamoto za Kijitonyama. Tunaenda kuzitatua ikiwemo changamoto za mto Kijitonyama, na baadhi ya barabara za mtaa.
Kijitonyama ndo Kata pekee Kinondoni yenye masoko makubwa manne, lakini pia ikiwa na vituo vikubwa vya daladala.
Tuna kituo kikubwa cha biashara, 'centre of Business'. Lakini pia uwanja wa soka wa KMC unaendelea kuinua maendeleo ya Wananchi.
"Tulipotoka huko nyuma sio sawa na sasa. Kwa sasa barabara za mitaa zipo safi, huduma za maji na Maendeleo mbalimbali" amemalizia Ndugu Amani Mohammed Barande.
Baadhi ya shamrashamra katika mkutano huo
![]() |
Msanii 'Mama Amina' nae alikuwepo kutoa burudani |
![]() |
drifting manjonjo ya kucheza na gari |
0 Comments