Na Matukio Daima Media
WANANCHI wa Mkuranga Mkoani Pwani wamesema wapo tayari kwa ushiriki wa uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 wakiwahimiza pia Vijana kutumia fursa hiyo na haki ya kikatiba ili kuchagua Viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo kwa miaka mitano ijayo.
Wananchi hao akiwemo Mzee Maulid Mwigange na Mariam Ngayonga wakati wakizungumza na Vyombo vya habari, wamewatoa wasiwasi pia wananchi na kwa kuwaeleza kuwa Oktoba 29, 2025 kutakuwa na usalama na amani ya kutosha kutokana na namna ambavyo serikali imejipanga kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata nafasi kamili na usalama wa kushiriki kupiga kura.
"Tutachagua Kiongozi anayetufaa na tumehamasika kushiriki kwasababu ya maendeleo mengi tu tunayoyashuhudia Mkuranga ikiwemo stendi nzuri na hatubugudhiwi." Ameongeza kusema Mohamed Makame, mwananchi na mfanyabiashara mdogo wa Mkuranga.
Kwa upande wake Habiba Jasmin, Kijana na mjasiriamali mdogo wa Mkuranga ametoa wito wa Vijana kutumia vyema fursa ya upigaji kura kuamua kuhusu hatma yao ya miaka mitano ijayo, akiombea kheri uchaguzi huo ili ufanyike na umalizike kwa amani ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku za uchumi.
0 Comments