Header Ads Widget

TAKRIBAN WATU 66 WAUAWA GAZA KATIKA SAA 24 ZILIZOPITA - HAMAS

 

Wizara ya Afya ya Palestina - Gaza inasema takriban watu 66 wameuawa na uvamizi wa Israel katika saa 24 zilizopita, na kuongeza idadi ya waliouawa katika Ukanda huo tangu 7 Oktoba hadi 67,074.

Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas inasema watu wengine 265 waliojeruhiwa wamefika katika hospitali za Ukanda wa Gaza katika muda huo huo.

Wizara hiyo inasema imekuwa vigumu kufikia watu ambao wamenaswa chini ya vifusi.

Ni nini kimekuwa kimetokea Gaza leo?

Milipuko kadhaa imeshuhudiwa huko Gaza mapema Jumamosi, huku mji wa Gaza ukikumbwa na mashambulio matatu tofauti ya anga, na kuua mtu mmoja, saa chache baada ya Trump kuitaka Israeli kuacha kushambulia Ukanda huo.

IDF imewaonya Wapalestina kwamba kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na karibu na Mji wa Gaza bado ni "eneo hatari la mapigano", na kuwataka tena watu kuhamia kusini.

Viongozi wa upinzani wameunga mkono mpango wa amani wa Trump na kumtaka Netanyahu kuunga mkono mpango huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI