![]() |
Mgombea Udiwani wa Kata ya Mbezi kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Ndg. Augustino Sanyaboma. |
Na Mwandishi Wetu, Ubungo.
MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Mbezi kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Ndg. Augustino Sanyaboma, amemshutumu mpinzani wake kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Pius Nyantori, kwa kushindwa kusimamia ipasavyo mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) wakati alipokuwa Meneja, hali ambayo amesema imesababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Akihutubia wakazi wa kata hiyo katika mkutano wa kampeni Mtaa Mshikamano, Sanyaboma alihoji uhalali wa Nyantori kuomba nafasi ya udiwani ilhali alishindwa kusimamia mradi muhimu uliokuwa ukihudumia maelfu ya wananchi kila siku.
"Wananchi wa Mbezi, Niseme au nisisemee?” aliuliza Sanyaboma, na wananchi kujibu kwa pamoja “Sema Baba!”
Huyu Nyantori (Pius) mnayeletewa kama mgombea wa CCM ndiye aliyekuwa meneja wa UDART. Changamoto na usumbufu mnaupata leo na kilichotokea kwenye zile vurugu wananchi wenye hasira kali kuyapopoa mawe mabasi ni matokeo ya uzembe wake wa Nyantori alipokuwa Meneja leo anataka kura zenu za udiwani je, kwa mikakati ipi ya kutatua matatizo ya Mbezi? wakati hata usimamizi wa UDART ulimshinda.!? Alihoji Sanyaboma.
Sanyaboma alisisitiza kwamba changamoto kubwa ya Kata ya Mbezi sio ukosefu wa fedha, bali ni uongozi wenye dhamira ya kweli kupigania maslahi ya wananchi.
Alifafanua kuwa Manispaa ya Ubungo hukusanya zaidi ya shilingi bilioni 40 kila mwaka kutokana na kodi na ushuru mbalimbali, na hupokea ruzuku kutoka serikali kuu takribani shilingi bilioni 95, hivyo kufikisha zaidi ya shilingi bilioni 140 kwa mwaka.
Ndugu zangu wa Mbezi Kiasi hiki cha fedha kinapogawanywa kwa kila kata, hakuna tatizo lisiloweza kushughulikiwa, hususan katika maeneo muhimu ya barabara, maji na afya. Wananchi wanachohitaji ni diwani jasiri wa kupigania maslahi yao kwenye Halmashauri, naomba mniamini mimi niko tayari kuwawakilisha kwa dhati,” amesema Sanyaboma.
0 Comments