Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
WAKAZI wa Bariadi Mjini wameanza maandalizi makubwa ya kumlaki kwa heshima ya juu Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye anatarajiwa kufanya ziara kubwa mkoani Simiyu Oktoba 10, 2025.
Katika maandalizi hayo, Mgombea Ubunge Jimbo la Bariadi Mjini kwa tiketi ya CCM, Mhandisi Kundo Mathew amekutana na wazee maarufu wa mji huo kwa kikao maalum cha kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mapokezi hayo.
Mhandisi Kundo amesisitiza kuwa ujio wa Rais Samia ni ishara ya heshima kubwa kwa mkoa wa Simiyu na fursa ya kuonyesha mshikamano wa kizalendo.
“Ni wajibu wa kila mmoja wetu kujitokeza kwa wingi kumpokea Mama yetu, na Mgombea Urais Dk Samia...zara yake ni alama ya upendo kwa wananchi wa Bariadi na uthibitisho wa dhamira yake ya kuwaletea maendeleo Watanzania,” amesma Mhandisi Kundo mbele ya wazee.
Pamoja na hilo, amewaomba wananchi kumpa Rais Samia kura za heshima ifikapo Oktoba 29, 2025, akibainisha kuwa kura hizo zitakuwa sauti ya kuthibitisha imani kwa kazi kubwa ya maendeleo inayoendelea nchini.
Mapokezi hayo yanatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambapo wananchi wote wamealikwa kushiriki kwa wingi kuonyesha mshikamano na mapenzi kwa kiongozi wa taifa.
Mwisho.


.jpg)







0 Comments