Header Ads Widget

RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USALAMA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA SIKU YA UPIGAJI KURA OKTOBA 29


Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Gabriel Makalla amewahakikishia wazee na wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa wamejipanga Vyema kuhakikisha siku ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kutakuwa na amani na mazingira tulivu ya upigaji kura, akitoa wito kwa kila Mwananchi mwenye sifa kujitokeza kwa wingi kuchagua Viongozi wanaowataka ili kuwaongoza kwa miaka mitano ijayo.


CPA Makalla ametoa wito huo wakati wa matembezi ya amani ya Wazee wa Mkoa wa Arusha, waliofanya matembezi hayo Jijini Arusha kwaajili ya kuliombea Taifa amani kama sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Wakianzia matembezi hayo kwenye Viunga vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kwenda Mnara wa saa, Metropole, Idara ya maji, kituo cha Mabasi Arusha na baadaye kumalizia tukio lao kwenye Viwanja vya Makumbusho Jijini Arusha.

"Kupiga kura ni haki ya Kikatiba ya kila Mtanzania. Wazee wangu mtukumbushe na kuwakumbusha Vijana kuitunza amani, kutumia vyema mitandao ya kijamii lakini Vijana wenye sifa za kupiga kura wajitokeze kwa wingi. Niwahakikishie mtapiga kura kwa amani na atakayeshinda atangazwe kushinda." Amesema.



Makalla amewahakikishia wananchi wote amani na usalama katika kipindi hiki cha lala salama za Kampeni, wakati wa upigaji kura na hata baada ya kura, akisema amani ni muhimu kwa maendeleo pamoja na ukuaji wa sekta ya utalii katika Mkoa huo ulio kitovu cha utalii kwa upande wa Tanzania bara.



Kwa upande wao baadhi ya wazee walioshiriki matembezi hayo kwaniaba ya wenzao wamewasihi wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuhimiza kila mmoja kulinda amani ya Mkoa wa Arusha, wakisema amani imekuwa tunu muhimu ya maendeleo na ustawi wa watu wa Mkoa wa Arusha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI