Header Ads Widget

RAIS WA IVORY COST,OUATTARA 83,AWANIA MUHULA WA NNE WA KITI CHA URAIS

 

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anawania muhula wa nne katika uchaguzi wa siku ya Jumamosi, akiahidi kuendeleza ukuaji thabiti huku wakosoaji wakilaani kile wanachoeleza kama jitihada za serikali yake za kukandamiza upinzani.

Uchaguzi katika nchi hiyo mzalishaji mkubwa wa kakao duniani unawakutanisha Ouattara, 83, dhidi ya mawaziri wawili wa zamani wa serikali pamoja na mke wa zamani na msemaji wa zamani wa mtangulizi wake, Laurent Gbagbo.

Ouattara ndiye mgombea pekee anayeungwa mkono na chama chenye nguvu cha kisiasa, na hivyo kumfanya kuwa kipenzi wengi.

Wapinzani wengine wawili mashuhuri, Gbagbo na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Credit Suisse Tidjane Thiam, walizuiwa kushiriki.

Ouattara, ambaye amepuuzilia mbali wasiwasi kuhusu umri na afya yake, aliingia madarakani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi minne baada ya Gbagbo kukataa kushindwa katika uchaguzi wa 2010.

Mwanabenki wa zamani wa kimataifa na naibu mkurugenzi mkuu wa IMF, Ouattara amesaidia kuiweka Ivory Coast miongoni mwa nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi katika kanda hiyo.

Amesimamia mageuzi ya kikatiba yaliyomruhusu kukwepa ukomo wa mihula miwili, na kuibua hasira ya wapinzani wake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI