Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini, kupitia CCM, Mhandisi Kundo Mathew ameendelea na mikutano ya kampeni kwa kuwaomba kura wananchi na kuwasisitiza kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili wafikishiwe huduma za Maendeleo katika maeneo yao.
Amewasisitiza kuwa endapo wamchagua Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Ubunge (Mhandisi Kundo) pamoja na Madiwani wa CCM wataboresha na kuimarisha utoaji wa huduma katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Barabara na Umeme.
Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya kampeni katika Mitaa ya Mwakibolo (kata ya Bunamhala), Ngogote (kata ya Mhango) na Somanda (kata ya Somanda), Mhandisi Kundo amesema kuwa serikali ya CCM imedhamiria kuimarisha utoaji wa huduma na kuboresha maisha na wanachi.
"Hakuna haja ya kuja na utitiri wa ahadi ambazo tutashindwa kuzitekeleza... CCM imejipanga kupitia Ilani yake kuwahudumia wananchi, kila kata tutafungua kilometa 50 za Barabara, Mradi wa Compact Mission 300 utamaliza tatizo Umeme na Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria nao ni Mwarobaini wa tatizo la Maji mjini Baeiadi" amesema Mhandisi Kundo.
Akiwa mtaa wa Ngogote, Mgombea huyo ameahidi kujenga zahanati, Barabara pamoja na Shule ili kurahisisha na kuwasogezea huduma wananchi ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.
Amesema kuwa atambua changamoto za wanafunzi na Wananchi hasa Wakina mama wajawazito kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya Elimu na afya, hivyo kupitia Ilani ya CCM watahakikisha huduma hizo zinawafikia wananchi.
Mwisho.














0 Comments