TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza siku ya jumatano Oktoba 29, 2025 kuwa siku ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Kwa Mujibu wa Tangazo hilo, wananchi wote wenye sifa kikatiba watapata fursa ya kuchagua viongozi watakaoongoza kwa kipindi kijacho Cha miaka mitano ijayo.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Mamlaka ya Sheria ya sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35 ameidhinisha siku hiyo kuwa siku ya MAPUMZIKO ya Kitaifa.
Uamuzi huyo unalenga kuwawezesha wananchi wote akiwemo watumishi wa Umma na wafanyakazi wa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura bila kikwazo.
Mwisho






0 Comments