Na Lilian Kasenene,Morogoro
Matukio DaimaApp
Taasisi ya kuimarisha uwajibikaji nchini ya (WAJIBU)imesaini mkataba wa makubaliano na Kituo cha Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC) wa kufanya utafiti kuhusu tathimini na mwitikio mdogo wa miradi ya ubia inayotekelezwa nchini.
Utafiti huo ukilenga kuongeza msukumo katika jitihada za serikali kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya miaka 25.
Akizungumza mkoani Morogoro mkurugenzi mtendaji wa kituo cha ubia wa sekta ya umma (PPPC)David Kafulila wakati wa kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya kituo Cha PPPC na taasisi ya kukuza mazingira ya uwajibikaji nchini ya WAJIBU.
Alisema Dira ya Maendeleo ya Taifa kama itategemea Kodi na mikopo pekee bila kuangalia maeneo mengine Tanzania haitawezakujenga uchumu wa nchi kufikia Dola zaidi ya tirioni Moja kama ilivyo kwenye malengo ya dira hiyo.
Makubaliano hayo pamoja na mambo mengine yatakayoangaliwa ni kufanya utafiti kuhusu tathimini ya mwitikio mdogo wa miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi nchini kwa kuangazia visababishi vikuu na suluhisho la vitenbo inayotekelezwa nchini.
Utafiti huo ukilenga kuongeza msukumo katika jitihada za serikali kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya miaka 25(TDV2050).
Kafulila alisema tafiti zitakazofanya zitasaidia kubadilisha masuala mbalimbali zikiwemo bajeti.
"Sisi kama kituo cha ubia napenda kutoa mwaliko na ushirikiano kwa taasisi yoyote ambayo inawiwa kufanya utafiti kwenye eneo hili lanubua na milango iko wazi na ndivyo tunavyojenga nchi na ni katika kufanya mabadiliko ya watu,"alisema.
Alitoa wito kwa vyuo vikuu vya umma na binafsi kuendelea kufanya tafiti zaidi kwenye maeneo yaliyopo na hiyo ni katika kutoa mchango kwa Serikali.
Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali CAG(mstaafu),ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU Ludovick Utouh alisema utafiti unaofanywa na WAJIBU kwa ushirikiano na PPPC unalenga kuchangia jitihada za Serikali ambayo ni maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo alipokuwa akizindua Dira hiyo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta hizo binafsi na umma.
"WAJIBU inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali vya awamu ya sita katika kuongeza mchango wa ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma katika kuleta Maendeleo ya nchi,"alisema.
Mwisho.
0 Comments