Header Ads Widget

POLISI WAANZA UCHUNGUZI KUHUSU KUTEKWA KWA POLEPOLE, WAKISISITIZA KUMUHITAJI KWA DCI




NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

Jeshi la Polisi nchini Tanzania, kupitia kwa Msemaji wake DCP David Misime, limesisitiza kuwa bado linaendelea kumsubiri Ndugu Humphrey Polepole ili aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia mitandao yake ya kijamii.

Ikumbukwe kuwa mnamo Jumatatu, Septemba 15, 2025, Jeshi la Polisi lilitangaza kuwa limefungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma hizo ambazo kada huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekuwa akizitoa.

 "Tuhuma ambazo ametoa na anaendelea kuzitoa, kulingana na jinsi alivyozielezea, zinaashiria uwepo wa makosa ya jinai kwa mujibu wa sheria, makosa haya yanahitaji ushahidi wa kuzithibitisha zitakapowasilishwa mahakamani.

Tuhuma hizo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii. Baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi, mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo au ushahidi na vielelezo vitakavyothibitisha tuhuma hizo hii ni kwa ajili ya kuwezesha hatua nyingine za kisheria kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria, na ndivyo utaratibu wa kisheria unavyotakiwa kuwa,” taarifa hiyo ya Polisi ilieleza.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa limeona taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa ndugu wa Polepole, zikidai kuwa alitekwa usiku wa kuamkia Oktoba 6, 2025. Polisi wamesema tayari wameanza kufanyia kazi taarifa hizo ili kubaini ukweli wa madai ya kutekwa kwake

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI