MATUKIO DAIMA MEDIA.
Mwanamuziki na mjasiriamali Sean "Diddy" Combs amehukumiwa kifungo cha miezi 50 jela na Mahakama ya Shirikisho jijini Manhattan, siku ya Ijumaa Oktoba 3, 2025, kwa kukiuka sheria za Marekani kuhusu usafirishaji wa watu kwa ajili ya ukahaba (Mann Act).
Awali, upande wa mashtaka ulitaka ahukumiwe zaidi ya miaka 11, huku mawakili wake wakitaka miezi 14 pekee, lakini Jaji Arun Subramanian aliona kiwango cha juu siyo cha haki, ingawa alimshtumu vikali Diddy kwa "unyanyasaji uliowasukuma waathirika kufikiria kujiua.'
Diddy mwenye umri wa miaka 55 alijutia kitendo chake akisema kilikuwa cha "aibu, cha kusikitisha na cha ugonjwa," huku akiomba msamaha.
Ingawa aliepuka kifungo cha maisha baada ya kuondolewa mashtaka ya RICO na usafirishaji haramu wa binadamu, sasa atakaa zaidi ya miaka mitatu gerezani kutokana na muda aliokwishotumikia wakati wa kesi.
Hata hivyo, bado anakabiliwa na kesi nyingi za madai na hasara kubwa ya kushuka hadhi na mali zake.
0 Comments