Lulu Mbwaga
Mwanza
Mfuko wa Taifa wa Hilifadhi ya Jamii NSSF, Mkoa wa Mwanza umefanya kongamano la waajiri kwa lengo la kutoa elimu ya mfumo wa utendaji kazi wa kidijitali unaoitwa NSSF PORTAL ambao utamsaidia muajiri na muajiriwa kuzifikia huduma za NSSF pasipo kufika ofisini.
Akifungua Kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilage, amepongeza uongozi wa NSSF Mkoa wa Mwanza, kwa kuandaa kongamano la waajiri, kwani kumekua na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi, hivyo changamoto za watumishi zitatatuluwa kutokana na kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu Sheria na kanuni za mfuko huo."Hakikisheni mnatekeleza kwa mujibu wa Sheria Kwa kwa kupelka mafao kila mwezi kwa wakati na kuhakikisha kuwa wafanyakazi wenu wanajiunga na mfuko wa kijamii utakao wasaidia hapo baadae" Alisema Mhe. Makilage.
Kwa Upande wake, Meneja wa mkoa wa Mwanza, Bwana Emmanuel Kahensa alisema kuwa, mfumo huo wa kidigital umerahisisha kwa muajiri kuingiza taarifa zake bila kufika ofisini, umerahisisha kuwasilisha michango ,urahisi wa kutoa huduma kwa wateja ,kumsajili muajiri mpya na mwajiri anaweza kuomba mafunzo kwa kupitia mfumo huo
Meneja wa Ukaguzi uandikishaji na Matekelezo Makao Makuu Bwana Cosmas Sasi
amesema kuwa mwaka 2018 NSSF ili lfanya maboresho ya Sheria na ikapewa jukumu la kuwahudumia wananchi waliojiari wenyewe, ambapo Shirika Hilo lilianzisha kampeni ya NSSF star wa mchezo ikiwa na lengo la kuwafikia wananchi wakiwemo wajasiriamali, Mama Lishe, Bodaboda, na wachimbaji wadogo wa madini
Nao, baadhi ya waajiri kutoka sekta mbalimbali akiwemo Ndg. Jackson Kaigamba na Bi. Vestina Malugu, wamesema kuwa mfumo wa NSSF PORTAL ni mzuri na unawarahisishia majukumu kwani awali walikua wanapoteza muda kwa kufika ofisini sambamba na Hilo wameshukuru wafanyakazi wa mfuko huo kwa kua tayari kuwasikiliza na kuwasaidia kutatua matatizo na kuwapa uelewa.
Ikumbukwe kuwa, Kongamano hilo, limefanyika October 20, 2025 katika ukumbi wa NSSF House Jijini Mwanza likiwakusanya waajiri 300 kutoka sekta mbalimbali.
0 Comments