Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA BUKOBA MJINI ATOA SALAMU ZA KRISMASI NA HERI YA MWAKA MPYA 2026

 


Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhe Johnston Mtasingwa ametoa salamu za heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2026 kwa viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama, pamoja na wananchi wote wa Jimbo la Bukoba.


Katika salamu zake, Mbunge Johnston Mtasingwa amewatakia heri viongozi wa Serikali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa Hajath Fatma Mwassa, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe Erasto Sima akiwatakia afya njema, amani na mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Kagera.

Aidha, ametoa salamu za heri kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya na Mkoa wa Kagera, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Dkt. Nazir Karamagi, akiwatakia mshikamano, busara na mafanikio katika kuendeleza chama na kuwatumikia wananchi.

Mwisho, Mbunge amewatakia wananchi wote wa Jimbo la Bukoba Mjini Krismasi njema na Heri ya Mwaka Mpya 2026, akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, umoja na mshikamano kwa maendeleo ya jimbo na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI