Header Ads Widget

WANNE JELA MIAKA SABA KWA JARIBIO LA KUMTEKA MFANYABIASHARA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Kinondoni, Dar Es Salaam imewahukumu Vijana wanne wakiwemo Mabondia wawili kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kumteka Mfanyabiashara Deogratus Tarimo, tukio lililoteka hisia za wengi Mitandaoni, wengi wakiwahusisha watu hao na Maafisa wa Vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Vijana hao waliohukumiwa ni Fredrick Nsato (21) Mkazi wa Kibamba, Isaack Mwaifuani (29) Mkazi wa Kimara, Benki Mwakalebela (40) na Bato Twelve (32) Mkazi wa Kimara Bonyokwa Mkoani Dar Es Salaam.

Kabla ya Hakimu Mkazi Mkuu Ramadhani Rugemalira kusoma hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Daisy Makakala amesema pamoja na kuwa hana kumbukumbu za makosa ya nyuma ya watuhumiwa wote wanne lakini anaiomba mahakama itoe adhabu sawa na kifungu cha sheria walichoshtakiwa nacho ili jamii ya Tanzania na dunia nzima ifahamu kuwa wanaotenda vitendo vya utekaji wa Raia wa makundi mbalimbali siyo Maafisa waJeshi la Polisi, bali ni watu wa kawaida ambao wamekuwa wakifanya vitendovya kiuhalifu kwa sababu mbalimbali.



"Naomba mahakama iwape adhabu kali washtakiwa kwa sababu vitendo vya utekaji vimeshamiri sana nyakati hizi, hali inayopelekea Jeshi la Polisi kulaumiwa kwa utekaji huo. Hawa watuhumiwa wangefanikiwa kumkamata Deogratius Tarimo akapotea asionekane Jamii ingeamini kuwa ni Polisi ndiyo wamempoteza hasa na vile wakati wanamkamata walikuwa wakijitambulisha kama Askari Polisi toka Kituo cha Gogoni wakati wakijua ni uongo. Hivyo ili kutoa fundisho kwa hawa watuhumiwa waliokutwa na hatia na jamii yote kwa ujumla mahakama iwape adhabu kali."amesema Wakili Makakala.


Kwa upande wao washtakiwa wao waliomba wapunguziwe adhabu na kudai kuwa wao walikuwa wanasaidia kumteka tu baada ya rafiki yao Frederick kuwaomba wamsaidie kumteka, kwa madai kuwa wanahisi Deo alitembea na mke wa rafiki yake Fredrick.


Kwa mujibu wa hati ya Mashtaka, Fredrick na wenzake walitenda kosa hilo Novemba 11, 2024 eneo la Kiluvya Madukani Lingwenye, lllilopo Wilaya ya Ubungo ambapo Ilielezwa kuwa siku hiyo ya tukio katika eneo hilo, washtakiwa kwa pamoja walijaribu kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo kwa nia ya kumuweka kizuizini isivyo halali ambapo Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani mahakamani hapo, Desemba 6, 2024 na kusomewa shtaka hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI