Header Ads Widget

NSSF LINDI, MATUMIZI YA TEHAMA YAMERAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA

 

NA HADIJA OMARY 

LINDI.....Mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Mkoa wa Lindi umezindua rasmi wiki ya huduma kwa wateja huku ikijivunia hatua kubwa waliyofikia Katika matumizi ya tehama ambayo yamerahisisha utoaji wa huduma kulingana na Kasi ya ukuwaji wa teknolojia duniani 

Akizungumza wakati wa uzinduzi  uliofanyika Katika ofisi za mfuko huo huko manispaa ya Lindi mkuu wa Wilaya ya Lindi victoria Mwanziva akatumia fursa hiyo kuwakumbusha waajiri kuhakikisha wanajiandikisha na kuwachangia wafanyakazi wao kwa mujibu wa Sheria 


Amesema Mfuko huo umejidhatiti kuwafikia waajiri wote ambao hawajajiandikisha na kuwachykulia Hatua stahiki wale wote wanaolimbikiza michango ya wanachama

Kwa upande wake Meneja wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Mkoa wa Lindi Bwana Juma Namuna amesema toka mfuko huo umeaza kutumia mfumo wa Tehama wameweza kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama wao


Amesema miongoni mwa manufaa wanayoyapata kutokana na mfumo huo ni pamoja na mfuko kuwawezesha wanachama kufungua madai ya mafao kwa njia ya mtandao ambapo imetoa fursa kwa wanachama walioko mbali na matawi ya mfuko huo kutolazimika kusafiri kufuata huduma hiyo

Wastaafu kuhakiki taarifa zao za mafao kwa njia ya mtandao , waajili kulipa michango Yao moja kwa moja kwa kutumia lango la waajiri (Employers portal)

" Kwa kupitia mfumo huu mwajiri pia anaweza malimbikizo yake ya michango na kuweza kupata namba ya malipo pasipo kulazimika kufika Katika Tawi la NSSF na hivyo kutoa muda wa uzalishaji"

 Afisa  wa hifadhi skimu kutoka  NSSF bwana shabani haule akiwasihi wananchi ambao sio waajiria kujiunga na mfuko huo ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na mfuko huo

Haule akaeleza mafao anayoweza kupata mchangiaji wa hiari ni pamoja na mafao ya kustaafu kwa mchangiaji aliechangia miaka kuanzia miaka 15, fao la huduma za matibabu, uzazi na  gharama za mazishi ya mchangiaji anapofaliki

Bi.Rosemeri Mroso ni miongoni mwa wachangiaji wa hiari ambae pia mnufaika wa mafao mbalimbali ikiwemo fao la huduma za Afya na uzazi amesifu uanzishwaji wa hifadhi hiyo ya skimu ambayo imekuwa faraja kwa kundi hilo lililojiajiri



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI