Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
Mgombea udiwani wa Kata ya Nshambya, Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, Bw Godson Gybson ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi wa kata hiyo, ikiwa atachaguliwa katika uchaguzi ujao
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika mtaa Wa bunkango Bw.Godson amesema.endapo atapata nafasi ya kuendelea kukitetea kiti chake Kwa nafasi ya udiwani vipo vipaumbele ambavyo tayari amevikamilisha kwa kipindi Cha uongozi wake akiwa diwani,huku akisema hatokuwa kiongozi wa kujifungia.
"Sitakuwa diwani wa kukaa ofisini. Nitakuwa diwani wa kuishi na wananchi, kusikiliza matatizo yao na kuhakikisha fedha za maendeleo zinatumika kwa uwazi na tija.
Aidha Bw Godson amesema Katika kuijenga Nshambya ataanzisha programu za kuwajengea uwezo Wananchi Wa kata hiyo hususani wanawake na vijana kuwainua kiuchumi kupitia vikundi vya uzalishaji na fursa mbalimbbali za ujasiriamali.
Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Kagera Ndg,Faris Buruhani alimpongeza Mgombea huyo kwa uamuzi wake wa kugombea, akieleza kuwa ni mfano wa vijana wanaojitokeza kuchukua nafasi katika uongozi ili kuleta mageuzi,na kuwasisitiza Wananchi kuendelea kuwa na Imani na kiongozi huyo.
“Chama chetu kinaamini katika nguvu ya vijana. Tunaona fahari kuona vijana wakijitokeza si kwa maneno bali kwa vitendo. Tunahitaji viongozi wenye maono ya kuleta maendeleo Kwa wote pia amewataka Wananchi kuwa na chaguo sahihi la kuchagua nani ataleta maendeleo yakulidhisha Kwa jamii.amesema Faris"
Mkutano huo ulihitimishwa kwa sala fupi ya amani, huku wananchi wakionesha mshikamano mkubwa kwa mgombea huyo, wakieleza matumaini yao kuwa anaweza kuleta mabadiliko yanayohitajika kwa muda mrefu katika Kata huyo.
0 Comments