Header Ads Widget

AHADI 10 ZA DKT. MWINYI KWA WAZANZIBARI

 

Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ameeleza vipaumbele muhimu vitakavyoongoza safari ya maendeleo ya Zanzibar katika miaka mitano ijayo endapo atapata ridhaa ya kuingoza Zanzibar kwa muhula wa Pili.

Vipaumbele hivyo vimejikita katika kuendeleza umoja wa Wazanzibari, kukuza uchumi jumuishi, na kuboresha maisha ya wananchi wote wa visiwani humo, sambamba na hilo vimekusudia kuimarisha misingi ya amani, ustawi, na maendeleo endelevu.

Vifahamu vipaumbele 10 vya Dk. Mwinyi kwa Wazanzibari;


1. Kuendelea kuwaunganisha Wazanzibari na kudumisha umoja, amani, utulivu, ushirikiano, maridhiano na uvumilivu.


2. Kujenga uchumi imara unaozingatia usawa na kunufaisha maeneo yote ya Zanzibar.


3. Kuimarisha upatikanaji wa ajira kwa vijana kwa kuzalisha ajira 350,000 katika sekta rasmi na isiyo rasmi ifikapo mwaka 2030.



4. Kuhakikisha uhakika wa chakula kupitia hifadhi ya Taifa ya chakula na kuongeza uzalishaji wa ndani.



5. Kuimarisha uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kwa mikopo, matumizi ya teknolojia, na mafunzo ya umahiri.


6. Kuanzisha makaazi bora na miji ya kisasa kwa kuzingatia teknolojia mpya ya ujenzi, mipango miji, na usafi wa mazingira.


7. Kuanzisha hifadhi ya kitaifa ya mafuta ili kuhakikisha upatikanaji endelevu na kupunguza athari za mabadiliko ya bei.


8. Kuweka vivutio maalumu vya uwekezaji katika sekta kuu za uchumi kama uchumi wa buluu, viwanda, kilimo na huduma.


9. Kuendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo elimu, maji na umeme.


10. Kuimarisha hifadhi ya jamii kwa wananchi wote.


Kupitia vipaumbele hivyo, Dk. Mwinyi anaendelea kuonesha dhamira ya kujenga Zanzibar yenye maendeleo ya kweli, usawa wa fursa, na ustawi wa kila mwananchi bila kuacha mtu nyuma.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI