
Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Itilima, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Njalu Silanga amewataka wananchi kuchagua viongozi wanaotokana na chama hicho ili waendelee kuchapa kazi na kuwaletea Maendeleo.
Njalu amewataka wananchi wenye sifa za kupiga kura kijitokea Oktoba 29, 2015 kumchagua Mgombea Urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, Mbunge (Njalu) pamoja na Madiwani wa CCM na kwamba waendelee kuwaamini ili viongozi hao wawaleteee Maendeleo.
Njalu ameyasema hayo jana kwenye mikutano ya Kampeni iliyofanyika kwa nyakati tofauti katika vijiji vyaa Gambasingu, Mwamanyangu, Nkololo na Nyamalapa ambapo ameeleza kuwa baada ya Uchaguzi serikali itahakikisha inaimarisha miundombinu ya Elimu, Maji, Afya, Umeme na Barabara.
Amesema Utekelezaji wa ilani ya CCM 2020/2025 umeonekana na Vitendo kwani sekta za Elimu, Afya Maji, Umeme, Barabara, Mawasiliano zimeimarishwa huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kuamini viongozi wanaotokana na CCM.
Mwisho.
0 Comments