Header Ads Widget

NJALU ANADI SERA ZA CCM KAMBI YA WATALII SOPER.

 

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Itilima kupitia CCM, Njalu Silanga (mwenye shati la kijani kulia) akiwa na wadau wa Utalii kwenye Kambi ya Soper.


Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Itilima kupitia CCM, Njalu Silanga amefika na kutembelea katika kitongoji cha Mwakubija, Kijiji Cha Ng'walali, kata ya Mwaswale wilayani Itilima Mkoani Simiyu kwa lengo la kusikiliza kero za wadau wa Utalii kwenye Kambi ya watalii iliyopo katika kitongoji hicho.


Akiwa ukingoni  kuhitimisha kampeni zake ndani ya Jimbo hilo, Njalu ametumia fursa hiyo kuomba kura na kunadi sera za CCM na kwamba ni mara ya kwanza kwa eneo hilo kupata fursa ya kusikiliza sera Mgombea wa Ubunge kwani awali walizoea kupiga kura bila kumjua Mgombea wanaempigia.


Wakizungumza na mgombea huyo, Wafanyakazi wa kampuni za utalii ndani ya hifadhi wameomba kutatuliwa changamoto za ubovu wa madaraja na ukosefu wa barabara kwenye baadhi ya maeneo ambayo yangewarahisishia wao kupata huduma za kijamii kwa uharaka, hali waliyoeleza kukwamisha shughuli za utalii na kuahatarisha maisha yao na Watalii nyakati za masika.




Akijibu maombi hayo, Njalu Silanga amesema tayari Chama Cha Mapinduzi kimebainisha kupitia Ilani yake juu ya kutatua changamoto hizo ambapo amesema endapo watakichagua chama hicho, barabara itafunguliwa kutoka hifadhini hapo hadi  wilaya ya Itilima na baadae mpaka Makao makuu ya mkoa wa Simiyu.




Aidha Njalu amewaomba kumpigia kura nyingi Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba wao wamekuwa mashahidi na wanufaika namba moja wa mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika Sekta ya Utalii na Rais Dk. Samia kupitia Royal Tour.



Njalu ameahidi kurejea tena kwenye eneo hilo baada ya uchaguzi huku akiwatoa hofu kua hakufika hapo kwa ajili ya kuomba kura pekee bali amefika kuwashukuru kwa kukupigia kura chama cha Mapinduzi katika chaguzi zilizopita licha ya kutofikiwa na wagombea wa nafasi mbalimbali.


Mwisho.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI