Header Ads Widget

NAYALANDU, AWAHAMASISHA VIJANA KUJITOKEZA OKTOBA 29 KUPIGA KURA.


 Na chausiku  said 

Matukio Daima Mwanza.

Zikiwa zimesalia siku takribani 5 vijana Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa wamehimizwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura litakalofanyika Oktoba 29, 2025, Nchi Nzima na kumpokea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufungaji wa kampeni zake za kugombea Urais kupitia chama Cha mapinduzi CCM Mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo oktoba 24, 2025 Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amewataka vijana kuwa mstari wa mbele na kujitokeza  katika zoezi hilo la kidemokrasia.


“Vijana sio Taifa la kesho, ni Taifa la leo. Tanzania ina vijana wengi kuliko rika lolote, hivyo wakitoka kupiga kura, Tanzania imepiga kura lakini pia alisisitiza kuwa siku ya uchaguzi ni “siku takatifu” ya kujichagulia viongozi wa ngazi za urais, ubunge, na udiwani.

Nyalandu aliwaomba vijana kuwasaidia wazee, wanyonge, na wakina mama kuhakikisha wanapiga kura, huku wakihakikisha amani na mshikamano unadumishwa na kubainisha kuwa kampeni za Rais Samia zimekuwa za amani, utulivu, na upendo nchi nzima, na sasa ziko kwenye hatua ya kumudu mjini Mwanza.

Aidha, alitangaza kuwa kesho atafanya kongamano na vijana wa kundi la Gen Z ili kuwasikiliza na kuwahamasisha kushiriki katika uchaguzi. Alisema ameshaongea na viongozi wa dini mjini Mwanza ili kuwahamasisha wananchi wao kujitokeza kwa wingi kupokea Rais Samia na kupiga kura.

Nyalandu alisisitiza umuhimu wa kulinda amani ya Tanzania na kueleza kuwa amani ni tunu adimu inayotamaniwa na mataifa mengi.

 “Amani yetu ni ya Mungu, na tunapaswa kuilinda kwa wivu mkubwa, Tusiruhusu mtu yeyote avunje amani hii na kuongeza kuwa uhuru wa kuabudu na kuishi unatokana na amani iliyopo Nchini.

Zoezi la uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, litaamua viongozi wa ngazi za urais, ubunge, na udiwani, huku chama cha CCM kikiendelea kushika nafasi ya uongozi katika siasa za Tanzania tangu uhuru.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI