NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
WANANCHI wamehimizwa kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu kupiga kura na kuwachagua viongozi watakao waongoza huku wakihakikishiwa swala la usalama ni mkubwa na hakuna maandamano yatakayofanyika.
Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Adam Best Simba wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika kata ya Shirimatunda manispaa ya Moshi.
Alisema kuwa, hakuna maandamano yatakayofanyika Oktoba 29 mwaka huu na usalama umeimarika hivyo yoyote mwenye kutaka maandamano labda akaandamane chumbani kwake na mkewe na watoto na sio vinginevo.
Mjumbe huyo alisema kuwa, wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani alitafuta maridhiano na vyama vya upinzani kutokana na nchi kuwa ya amani lakini sasa viongozi wa vyama hivo hawajulikani wanachotafuta.
Mwisho..
0 Comments