Na Moses Ng'wat,Songwe.
MIRADI 43 ya maendeleo yenye thamani ya Sh 20.5 bilioni inatarajiwa kuzinduliwa, kutembelewa, kukaguliwa na kuweka mawe ya msingi na mbio za mwenge wa uhuru Mkoani Songwe kwa mwaka 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Jabir Omary Makame amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Oktoba Mosi,2025, kuhusu maamdalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru Oktoba 2,2025 katika kijiji cha Kamsamba kata ya Kamsamba wilayani Momba ukitokea mkoani Rukwa.
Makame amesema katika Mkoa Songwe mwenge wa uhuru unatarajia kukikbizwa kilomita 623 katika halmasauri zote tano za mkoa huo ambazo ni Momba, Tunduma, Ileje, Mbozi na Songwe.
Amesema Oktoba 2, 2025 mwenge wa uhuru utazunguka Halmashauri ya momba, Oktoba 3,2025 utazunguka Halmashauri ya mji wa Tunduma, Oktoba 4, 2025 Halmashauri ya Ileje, Oktoba 5, 2025 Halmashauri ya Mbozi na Oktoba 6, 2025 Halmashauri ya Songwe ambapo Oktoba 7,2025 mkoa wa Songwe utakabidhi mwenge wa uhuru katika mkoa wa Mbeya.
Makame amesema miradi hii imetekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali kuu, halmashauri za wilaya, wahisani, Pamoja na wananchi.
"Fedha hizii Sh 20.5 bilioni ambazo mwenge wa uhuru utapitia miradi ni sehemu ndogo ya fedha ya zaidi Sh 700 bilioni ambazo wananchi wa mkoa wa songwe zilizotolewa ma serikali ya awamu ya sita katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imesaidia sana katika kuleta mabadiliko ya wananchi na kuboresha Maisha yao ya kila siku'," amesema Makame
Makame amewataka wananchi wa mkoa wa Songwe kujitokeza kwa wingi kuupokea mwenge wa Uhuru October 2, 2025 n kujitokeza maeneo ambako utakagua, kuzindua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi.
Kauli mbiu ya mwenge Mwaka huu inasema "Jitokeze kushiliki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu"
Pia Makame amesema kulingana na kauli mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2025 kwa mkoa wa Songwe kampeni zinaendelea vizuri na hakuna changamoto zilizojitokeza kuathiri vyama vya siasa kwenye michakato ya mikutano ya kampeni.
Makame amewasihi wananchi kujitokeza kushiriki kwa wingi kupiga kura kuchagua viongozi wao siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 29,2025.
Roina Sikaluzwe mkazi wa kata ya Chiwezi wilaya ya Momba amewasihi wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi kupokea mwenge wa uhuru kwani unatarajia kuzindua kituo cha afya kata ya Chiwezi ambacho kwa ukanda huo ni kituo pekee cha afya kitakachokuwa kinatoa huduma kwa wananchi.
Mwisho.
0 Comments