Header Ads Widget

MWANAMKE ATEKETEZA NYUMBA KOREA KUSINI KISA KUUA MENDE


 Polisi wa Korea Kusini wamesema wanatafuta kibali cha kumkamata mwanamke aliyesababisha moto katika jengo lake la makazi wakati akijaribu kumuua mende kwa kutumia kifaa cha kutengeneza moto kama kifaa cha kuteketezea, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

Jirani mmoja wa mwanamke huyo alipoteza maisha baada ya kuanguka kutoka ghorofani katika jaribio lililoshindikana la kutoroka kupitia dirisha.

Mwanamke huyo, ambaye yuko katika umri wa miaka ya ishirini, aliwaambia polisi kuwa alijaribu kumchoma mende kwa kutumia kiberiti na dawa inayowaka moto, na kuongeza kuwa amewahi kutumia mbinu hiyo hapo awali.

Hata hivyo, siku ya Jumatatu, baadhi ya vitu ndani ya nyumba yake vilishika moto.

Polisi katika jiji la kaskazini la Osan wamesema mwanamke huyo anaweza kufunguliwa mashtaka ya kusababisha moto kwa bahati mbaya na kusababisha kifo kwa uzembe.

Kuchoma mende kwa kutumia vifaa vya kulipua moto iwe ni tochi au vifaa vya kutengeneza moto nyumbani kumekuwa mbinu mpya ya kuondoa wadudu wa nyumbani, ikienezwa kupitia video katika mitandao ya kijamii.

Mwaka 2018, mwanaume mmoja nchini Australia aliteketeza jikoni mwake alipokuwa akijaribu kuwaua mende kwa kutumia kifaa cha kutengeneza moto kutokana na dawa ya kuua wadudu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI