
Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia CCM, Mhandisi Kundo Mathew ameahidi kusimamia na kuuboresha miundombinu ya Masoko na ujenzi wa Barabara za Mitaa katika Mji wa Baruadi endapo atachaguliwa kuwa Mbunge Oktoba 29, 2025.
Aidha, Mhandisi Kundo amewataka wananchi kump kura za kishindo Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Madiwani ili waendelee kuwatumikia kwa muda wa miaka mitano ijayo.

Akizungumza kwenye mikutano ya Kampeni iliyofanyika kwenye mitaa ya Sima (kata ya Sima) na Kidalimanda (kata ya Bunamhala), Mhandisi Kundo amewasisitiza wananchi kujitokeza kupiga kura ili kuhalalisha viongozi watakaowaletea Maendeleo.
"Hakuna nchi yoyote iliyoendelea bila kufungua Barabara zake, tukijenga miundombinu mizuri tutafungua fursa ya uchumi, biashara, usafiri na usafirishaji wa mazao, tutaweka taa za Barabarani ili Wakina mama wafanye Biashara pia tutafungua Barabara za mitaa...Mto ndoba tutajenga daraja la juu ili kuondoa adha ya maji, tupeni kura tuboreshe masoko na Barabara" amesema.
Katika hatua nyingine, Mhandisi Kundo amesema serikali imepanga kujenga kituo Cha Afya Bunamhala ili wananchi wasitembee umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu, pia baada ya Uchaguzi watafungua barabara ya kidalimanda kwenda Luguru na Kidalimanda kwenda Sakai.
Mhandisi Kundo ametumia mikutano hiyo kuwanadi na kuwaombea kura Wagombea Udiwani wa CCM kutoka kata za Sima (Zebedayo Kingi) na kata ya Bunamhala (Nkamba Zabron).
Mwisho.
0 Comments