Header Ads Widget

AMEIR HASSAN ATOA AHADI YA POSHO YA LAKI TANO KWA KILA MZANZIBAR

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA,ZANZIBAR, KIKWAJUNI 

Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Demokrasia Makini, Ameir Hassan Ameir, ameahidi kutoa posho ya shilingi laki tano (500,000) kila mwezi kwa kila Mzanzibari endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Kikwajuni, Mjini Magharibi Unguja, Ameir alisema hatua hiyo ni sehemu ya mpango wake maalum wa kuinua hali ya maisha ya wananchi na kuhakikisha kila Mzanzibari anaishi maisha bora.

“Nimeamua kugombea nafasi hii kubwa katika nchi yetu nikiwa na dhamira ya dhati ya kutoa mchango wangu katika kusaidia Wazanzibari waishi maisha mazuri. Ndiyo maana nimekuja na mpango wa kutoa posho ya laki tano kwa kila mwezi mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Zanzibar,” alisema Ameir.

Mgombea huyo alisisitiza kuwa mpango huo si ndoto, bali ni dira ya kweli inayotekelezeka kwa kufanya kazi kwa bidii na kupanga vipaumbele sahihi vya maendeleo.

Ameir alibainisha kuwa ili kufanikisha azma hiyo, serikali yake itajikita katika ukuaji wa uchumi kupitia sekta muhimu ikiwemo Utalii, Kilimo cha kisasa na hai, Uvuvi, Elimu na Ujuzi, pamoja na Viwanda vidogo na vya kati.

Aidha, aliahidi kuboresha miundombinu ya kiuchumi na kuwekeza katika maeneo yatakayoongeza pato la Taifa, akisisitiza kuwa Zanzibar ina rasilimali nyingi ambazo zikitumika vizuri zinaweza kubadili maisha ya wananchi wote.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI