Header Ads Widget

KIBONDE; AHAIDI MASHAMBA BURE KWA VIJANA NCHI NZIMA.

Na Shemsa Mussa -Matukio Daima Media 

BUKOBA, KAGERA –

Mgombea urais kupitia Chama MAKINI, Coaster Jimmy Kibonde, amezungumza na wakazi wa Bukoba mkoani Kagera, ambapo amawaeleza vipaumbele vyake vikuu endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Awamuya Saba Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akihutubia umati wa wakazi wa Bukoba, Kibonde amesema kuwa serikali yake itaweka msisitizo kwenye sekta tatu kuu: elimu, afya na kilimo, akiamini kuwa msaada mkubwa kwa Mtanzania ni kumpatia elimu bora bila malipo kufanya hivo ni kusaidia na kumkomboa mtanzania 

Ameongeza kuwa serikali yake itahakikisha wanafunzi wote wanaofaulu na kupata nafasi ya kuendelea na elimu ya juu, hata katika nchi za nje, watafadhiliwa kwa masharti ya kurudi nyumbani na kuwatumikia wananchi kwa manufaa ya taifa.

Katika kusaidia ajira kwa vijana, Kibonde ameahidi kuwapatia vijana wote wenye umri kati ya miaka 21 hadi 31 mashamba yenye ukubwa wa ekari tano kila mmoja, yakiwa na hati miliki halali. Mashamba hayo yatawawezesha vijana kupata mikopo ya kilimo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha.

“Tukiwapa ardhi na hati miliki, tunawawezesha vijana kuanzisha maisha yao na kuchangia uchumi wa taifa na tukifanya hivo basi Kila kijana mwenye ardhi anaweza kukopeshaka sehemu yoyote Kwa sababu tayari ana kitu Cha kuzamini,” amesema.

Katika upande wa viwanda, Kibonde ameahidi kuanzisha viwanda vya kuzalisha pembejeo za kilimo ambavyo vitakuwa chini ya usimamizi wa serikali. Pembejeo hizo zitasambazwa kutoka kwenye maghala ya serikali moja kwa moja hadi mashambani kwa urahisi zaidi Kwa mkulima .

Aidha, Kibonde ameweka bayana kuwa serikali yake itawekeza kwenye kufufua mazao ya kimkakati kama kahawa, chai na pareto, na kuhakikisha mkulima ananufaika moja kwa moja kupitia bei nzuri na matumizi ya mashine za kisasa mashambani.

Kwa ujumla, Kibonde ameahidi serikali yenye kujali maendeleo ya mtu mmoja mmoja, hasa kupitia elimu, afya bora na kuinua sekta ya kilimo kama kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI