Header Ads Widget

HALI YA WASIWASI YAONGEZEKA NCHINI CAMEROON,SERIKALI YAWAKAMATA WAANDAMANAJI KADHAA

 

Serikali ya Cameroon inasema waandamanaji kadhaa wametiwa mbaroni katika mji wa kaskazini wa Garoua, ngome ya mgombea wa upinzani Issa Tchiroma Bakary, huku kukiwa na hofu kuhusu uwezekano wa ghasia nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Waziri wa Mambo ya Ndani Paul Atanga Nji alisema "wasumbufu" waliokamatwa walitumiwa na wachochezi kutoka ndani na nje ya nchi. "Kati ya watu waliokamatwa, 20 watapelekwa katika mahakama za kijeshi kujibu kwa vitendo vya uasi na uchochezi wa uasi," Nji alifichua, akiongeza kuwa wengine walipelekwa katika mji mkuu wa Yaoundé kwa uchunguzi zaidi.

Hatua hiyo inafuatia mfululizo wa maandamano huko Garoua na Yaoundé leo, ambapo washiriki walishutumu hitilafu za uchaguzi na kueleza kumuunga mkono Tchiroma ambaye alidai ushindi katika uchaguzi wa rais.

Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha makundi yakiandamana na mabango yenye picha ya msemaji wa zamani wa serikali ambaye sasa anataka kumvua madaraka mkuu wake wa zamani Paul Biya.

Maafisa wa utawala katika tarafa ya Benoue ambako Garoua iko, wamepiga marufuku mzunguko wa pikipiki za kibiashara kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na moja asubuhi kwa saa za ndani.

Ilifuatia maandamano ya Jumatatu usiku na mamia ya waendesha baiskeli ambao waliingia barabarani katika kuonesha uungaji mkono kwa Tchiroma, kiongozi wa chama cha Cameroon National Salvation Front.

Katika siku za hivi karibuni, maafisa wa utawala, watawala wa kimila, mashirika ya kidini na ya kiraia wameomba utulivu wakati nchi ikisubiri matokeo ya uchaguzi wa urais.

Huku wengi wakiazimia kutetea kile wanachodai ukweli wa kura, kuna wasiwasi kwamba huenda taifa likakumbwa na misukosuko ya baada ya uchaguzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI